Makala
MUNGU KUINUA WATU KWAAJILI YAKO
| Makala
Isaya 43:4
Isaya 43:4 “Kwa kuwa ulikuwa wa thamani machoni pangu, na mwenye kuheshimiwa, nami nimekupenda; kwa sababu hiyo nitatoa watu kwa ajili yako; na kabila za watu kwa ajili ya maisha yako.” Ingawa upo katika hali ya maumivu na dhambi lakini kumbuka Mungu anakupenda na kukuheshimu, anakuchukulia wewe kama kitu chake cha thamani. Hivyo haijalishi una changamoto kiasi gani weka hili katika akili yako ya kwamba MUNGU ANAKUPENDA, ANAKUTHAMINI na KUKUHESHIMU kwa sababu wewe ni wa THAMANI machoni pake.
Mambo haya yasiondoke katika akili yako, usijiwazie hasi bali waza chanya, jisemeshe moyoni mwako kuwa wewe ni mtu unayependwa na Baba yako wa Mbinguni, unaheshimiwa na ni wa thamani machoni pake, alikuumba kwa ajili yake na alikuumba kwa utukufu wake. Unapo tangaza na kukiri hayo unaumba mazingira mazuri mbinguni kwa ajili yako, kwa maana kila aliye zaliwa mara ya pili yaani (aliye okoka) ni kwa ajili ya Utukufu wa Mungu.
© Pastor Innocent Mashauri – MADHABAHU YA SIRI ZA BIBLIA
+255 758 708804 Whatssap call and text anytime
SADAKA